Heri ya mwaka mpya, 2015!

Asalaam Aleikum!

Kama mjuavyo nyote mwaka wa 2014 ndo umekwishamalizika na tumeuanza mwaka mpya kabisa. Kwanza natumai sote tumefika na tumeuona. Pili natumai malengo yetu yote ya 2014 tuliyatimiza na tumekwishajipangia malengo makubwa zaidi kwa mwaka huu mpya. Mimi binafsi nilidhamiria kuanzisha tovuti yangu inayohusiana na mambo ya lugha hapa Tanzania na ninashukuru nilifanikiwa kwa hilo. Kilichobaki sasa ni kuhakikisha tovuti hii inafanikiwa.

Sijui nyinyi wenzangu mna mipango gani kwa ajili ya 2015, ila ninawatakia nyote mafanikio mema na inshallah sote tuweze kufika tena tarehe kama hii hii mwakani.

Mungu awabariki nyote, Mungu aibariki funlughaswahili.com!

Amin!