Translation Challenge #10… (swa-eng)

Been more than a month since I last posted anything, what can I say I’ve been busy…chasing paper, in Swahili we say “nakimbiza mshiko”
Thanks to Michael Theys for bringing it to my attention that my website was down, apologies if you couldn’t access it for the past few days-I saw it but ignored it as just another little something that will sort itself out in a few hours, bad idea!
Anyways I was going to post something totally different then changed my mind at the last minute and now we are gonna do some translating. Am gonna talk to you about something I discovered today that really made my day. Here goes…

Kama umewahi kuishi Dar, maeneo ya Mbezi Beach utakuwa umegundua kwamba kuna kero moja inayotuudhi sana wakazi wa huku. Kero hii ni ukosefu wa sehemu ya kufanyia mazoezi, maarufu kama ‘gym’. Tangu nirudi Dar, takriban miezi minane iliyopita, nimekuwa nikitafuta sehemu ya kufanyia mazoezi bila mafanikio. Ikanibidi hata nijiunge na ‘gym’ moja iliyopo maeneo ya Oysterbay ambapo ni mbali na kwetu na matokeo yake sikuweza kufanya mazoezi mara tano kwa wiki kama nilivyopanga. Mwisho wake nilipoteza fedha zangu jambo ambalo liliniuma sana.

Basi hivi leo nimetembelea jengo moja jipya huku maeneo ya kwetu na kuona tangazo la kufunguliwa gym kwenye ghorofa ya juu ya jengo hilo. Tangazo lilisomeka “opening soon”! Yani furaha yangu haiwezi kuelezeka, na nina hakika wakazi wengi wa Mbezi Beach hasa sisi kina dada wenye miili isiyoturidhisha tumefurahi mno! Asanteni sana “Body Line” kwa kusikia kilio chetu na kutuletea mkombozi.

Mazoezi hoyee!