Translation Challenge #8…(swa-eng)

Mvua za Bongo:

Miaka saba imepita tangu niondoke nyumbani, nimerudi hivi majuzi tu. Loh! Niliyoyaona yameniacha kinywa wazi! Wahenga walisema ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni, ama kweli nimeyaona.

Hivi karibuni msimu wa mvua za masika ulianza. Basi kero tunazozipata wakazi wa Dar ni kubwa sana. Matope kila unapokwenda, foleni za magari zisizoisha, maji machafu kujaa barabarani, madaraja kuvunjika na mito kufurika na kusababisha wanaoishi bondeni kulazimika kuhama kwani mali zao zote aidha zimesombwa au kuharibiwa na maji.

Kibaya zaidi hali hii haibadiliki kila mwaka ni yale yale. Viongozi wetu wanazidi kutuangusha kwa hili. Miundombinu ni mibovu na haifai kwa karne hii ya ishirini na moja. Tunaomba tu Mola uchaguzi mkuu ukifika mwakani wananchi wawapigie kura viongozi watakaotuokoa na haya majanga yanayosababishwa na mvua. Mungu ibariki Tanzania.

Translation Challenge #5… (swa-eng)

Hivi majuzi nilitembelea duka la kampuni moja maarufu ya simu hapa Dar maeneo ya kwetu, ili nisaidiwe kupata huduma ya mtandao wa intaneti. Wafanyakazi niliowakuta kwa kweli walikuwa ni wavumilivu na wachangamfu sana. Walinipa huduma ya hali ya juu mpaka nikajisikia kweli mimi ni mfalme (kama usemavyo msemo maarufu kuwa “mteja ni mfalme”). Read More