Translation Challenge #9… (swa-eng)

2014-05-17-21-57-11--1638277407

Jana nimebahatika kutazama filamu moja yenye asili ya Kichina iitwayo “Under The Hawthorn Tree”. Filamu hii inatokana na kitabu kimoja maarufu sana chenye jina hilo hilo ambacho kimeuza nakala zaidi ya milioni moja nchini China tu.

Kwa ufupi hadithi inaelezea mapenzi kati ya msichana mdogo maskini na mvulana aliyetoka kwenye familia yenye uwezo wakati wa miaka ya sabini nchi ya China ilipokuwa kwenye kipindi kigumu cha mapinduzi.

Kwa kweli filamu hii ni nzuri mno na waigizaji wakuu walifanya kazi ya kusifika kabisa. Kama hujaitazama au kusoma kitabu cha hadithi hii ningekushauri ufanye hivyo na nakuahidi utakuja kunishukuru. Ila nikupe tahadhari moja tu-hakikisha una kleenex mkononi kwa sababu ninakuhakikishia utaihitaj!