Translation Challenge #5… (swa-eng)

Hivi majuzi nilitembelea duka la kampuni moja maarufu ya simu hapa Dar maeneo ya kwetu, ili nisaidiwe kupata huduma ya mtandao wa intaneti. Wafanyakazi niliowakuta kwa kweli walikuwa ni wavumilivu na wachangamfu sana. Walinipa huduma ya hali ya juu mpaka nikajisikia kweli mimi ni mfalme (kama usemavyo msemo maarufu kuwa “mteja ni mfalme”). Baada ya siku chache nilirudi nisaidiwe mara nyingine tena na kama kawaida yao walinipa huduma nzuri sana. Kaka zangu wawili pamoja na dada, kama wasemavyo watoto wa mjini, nimetokea kuwapenda bure tu! Asanteni sana kwa huduma zenu nzuri na za kuridhisha. Nitarudi tena!

IMG_0034

Tagged , . Bookmark the permalink.

2 Responses to Translation Challenge #5… (swa-eng)

 1. madebe says:

  Here is my translation attempt….

  Just recently i visited the shop of a well known phone company here in my part of Dar, seeking help in relation to the internet. I found the shop assistants both very patient and cheerful. In fact they gave me such good service that i felt like a ‘king’ (as in ‘the customer is king’). After a few days I again needed to return to the shop and just like before received excellent service. I left the shop loving my two elder bothers and sister, as they say in the city. Thank you all for keeping the customer satisfied. I’ll be back again.

  Felt like i became a little too literal with the last couple of sentences….

 2. lisensei07 says:

  Hi Madebe, really good job! You are right the last bit ‘umeboronga kidogo’ 😉 It should be, “my 2 brothers and sisters, as the youth in town would say, I have come to love you without reason”.
  Good stuff!

Leave a Reply