Translation Challenge #6… (swa-eng)

Nina furaha sana kusherehekea mwaka mmoja tangu tovuti hii kuanzishwa. Kusema ukweli sikuanza na matarajio makubwa, nilitaka tu kuwaonyesha wanafunzi wangu sampuli za mbinu ninazotumia kufundisha na pia kuwapa watu wasiojua Kiswahili ladha kidogo tu ya lugha hii, yani tunaita kionjo. Mwanzoni watu walikuwa wanakuja tu wanachungulia wanaondoka, bila hata kuniachia mawazo yao. Ila sasa nafurahi sana ninapoona watu wanaambiana juu ya tovuti hii, wanawasiliana nami kupitia mitandao ya jamii na wengine hata kuniweka kwenye orodha ya vifaa vya kujifunza Kiswahili (http://www.fb10.uni-bremen.de/khwagner/swahili/links/gesamt.aspx, http://kamusi.org/content/swahili-learning-resources)……sielewi Kijerumani ila natumaini wameandika mambo mazuri tu!

Asanteni sana kina Boga, Joyce Keeley, Madebe na wengine wote wanaozidi kutembelea na kurusha maswali, “komenti” nk. zinazonisaidia kuboresha ninachokiandika hapa. Inshallah tutasherehekea hata miaka kumi na zaidi ila kwa sasa ntashukuru tu tukifikisha mwaka wa pili.

Mungu ibariki Fun-Lugha!

Tagged , . Bookmark the permalink.

5 Responses to Translation Challenge #6… (swa-eng)

 1. fun~lugha says:

  Ya leo ndefu kidogo, niwieni radhi!

 2. madebe says:

  Usijali ninakupartia radhi. Lakini naomba usubiri jaribio yangu mpaka kesho.

 3. fun~lugha says:

  He he! Nashukuru

 4. madebe says:

  I am very happy to celebrate one year since i started this website. To be truthful i didn’t begin with high expectations, i just wanted to show my students an example of the method i used to teach and also to give those who don’t know kiswahili a small taste of this language, that is a sample . To begin with people just came to check it out then they left, without even letting me know their thoughts. But now it makes me very happy when i see people tell each other on about this website, they communicate with me through the internet and even others have put me on lists of the best sites to teach yourself Kiswahili (http://www.fb10.uni-bremen.de/khwagner/swahili/links/gesampt.aspx)….i dont understand German so i just hope what they write is complimentary!
  A big thanks to Boga,Joyce Keeley,Madebe and all those who have visited and asked questions,made comments etc. These help me make what i write better. God willing we will celebrate even ten or more years but for now i am am just grateful we have reached the second year.

  New words for me were
  Tovuti
  Matarajio
  Mbinu

  Also
  niwieni

  I used the kamusi for these words, but still niwieni was problematic with wi being wicked/evil/bad i was unsure of the -eni, but from context i guessed at I’m bad (of course is a good way) sort of ..felt naughty.. ie In relation to a perceived indulgence say in chocolate, or maybe an extra portion of samaki with tui la nazi

 5. fun~lugha says:

  Hey! The phrase is niwie radhi which is just a way of apologizing. When I add the ni at the end its just to show that am referring to many people. You can read on that in LESSON #70. Glad you picked up all that vocab, be sure to put it to good use now!

Leave a Reply